FB_IMG_1515403583797

Zaidi ya vijana 2000 wanaendelea kupata Maarifa na kuongeza zaidi THAMANI katika maisha yao. Unataka kuwa mmoja wao?

Katika maisha yako, kuna wakati unahitaji msaada na Ushauri wa kitaalamu ili uweze kusonga mbele. Iwe ni katika kukabiliana na Mambo yaliyopita, kuacha Tabia zisizofaa, kuweka Malengo, kuboresha mahusiano yako, kukabiliana na Hasira au kutafuta kujua kusudi halisi la wewe kuletwa hapa duniani……..Inaleta matumaini sana pale unapokuwa na mtu wa kukusaidia na kukuongoza katika kukabiliana na changamoto hizo kutokana na ujuzi alionao.

Utakapofanya uamuzi wa kupata Mwongozo, Mafunzo na Ushauri wa kitaalamu katika eneo linalokusumbua, kamwe hautajutia.

Utapatiwa ushauri wa kitaalamu na Mafunzo muhimu yatakayokusaidia kupata majibu sahihi ya maswali na changamoto mbalimbali unazopitia katika maisha yako.

Kesho yako inategemea sana aina ya maamuzi utakayoyafanya leo. Anza sasa, wakati ndio huu.

KUPATA HUDUMA YA USHAURI (BURE)

Ushauri wa Ana kwa Ana (Mtu Binafsi)
One- on- one Coaching.

Huduma hii ni kwa ajili ya mtu Binafsi. Utapata Fursa ya kuzungumza na Mwalimu kwa Faragha na uhuru zaidi.

Mwalimu atashirikiana na wewe bega kwa bega katika kutafuta suluhu ya changamoto zako, kuweka Malengo mbalimbali na kusimamia hatua za mabadiliko yako kila siku.

Kikundi cha watu 4 - 10
Group Coaching

Hii ni huduma Maalumu kwa ajili ya kikundi kidogo cha watu. Kikundi cha watu wasiopungua 4 na kisichozidi watu 10, wenye Malengo yanayofanana, watapatiwa Mafunzo na Ushauri wa kitaalamu katika maeneo wanayohitaji kupiga hatua.

Hapa kila mmoja anapata Fursa ya Kujifunza kutoka kwa mwenzake, kubadilishana ujuzi na kuongeza ushirikiano zaidi.

Semina

Huduma hii ni kwa ajili ya Taasisi au Watu ambao wanataka kufanya mabadiliko katika maisha yao binafsi au ya kitaasisi, wanaotaka kufikia malengo yao, kuongeza ufanisi na utendaji katika nyanja mbalimbali za kitaaasisi au kibinafsi.

Mafunzo Maalumu kwa Vitendo
Coaching Workshops

Hii ni huduma ya mafunzo maalumu (Kwa ajili ya Kutatua changamoto moja) ya vitendo ambayo yanaweza kudumu kwa muda siku moja hadi siku tatu mfululizo. Pamoja na muda wa mafunzo kutofautiana, washiriki daima wataondoka na angalau mbinu chache zitakazowasaidia katika kukabiliana na changamoto zao mbalimbali.

Public Speaking

Katika Mikutano Maalumu ya Vikundi au Taasisi, Mwalimu huandaa Mada maalumu kutokana na uhitaji wa Kikundi au Taasisi husika kwa ajili ya Kufikisha ujumbe na Maarifa kwa kwa walengwa.

FANYA UAMUZI SAHIHI LEO.

Hapa ni Sehemu sahihi kabisa ya kutafuta Suluhu ya Changamoto zako na Kupata Fursa ya Kufanya mabadiliko chanya katika maisha yako.

  • Unapata Changamoto katika kuweka Malengo na kuyafikia kwa wakati?
  • Fikra na Mitazamo Hasi vimekuwa kikwazo cha wewe kupiga hatua katika maisha yako?
  • Mahusiano yamekuwa ni kikwazo cha Maendeleo katika Maisha yako na hujui nini cha kufanya?
  • Unashindwa kuhimili Hofu, Uoga, Wasiwasi na Hasira katika maisha yako?
  • THAMANI yako inapotea kwa kushindwa kufahamu kusudi lako halisi la kuletwa duniani?
  • Unaipenda FURAHA lakini haidumu katika Maisha yako?