All posts by: Coach Ansey

by in MAISHA NA MALENGO

ANGALIA USIJE KUJUTA MIAKA 10 IJAYO (MAAMUZI YANAYOWEZA KUKUPA MAJUTO BAADAE).

Maisha yetu kama binadamu ni mafupi sana, hivyo tunapaswa kuwa makini sana katika kufanya maamuzi mbalimbali yatakayoongoza maisha yetu ya sasa na baadae. Ni wazi kwamba, hakuna anayeweza kufanya maamuzi sahihi wakati wote na kuepuka kufanya makosa lakini ni muhimu sana kuhakikisha unajilinda kwa kuepuka kufanya maamuzi yatakayokufanya ujutie na kupata maumivu moyoni. Vijana tuliopo […]

by in MAISHA NA MALENGO, THAMANI

KWANINI UNAPASWA KUWA NA DIARY KWA AJILI YA MAISHA YAKO?

Wengine wanaita Diary, wengine Journal n.k, kila mmoja anaweza kuita jina lake kutokana na aina ya matumizi binafsi. Lakini katika yote, “Diary/Journal” ni mfano wa daftari unaloweza kuandika mambo yako muhimu ambayo mtu mwingine hapaswi kuyaona. Kamwe usiidharau nguvu ya Diary/Journal kutokana na faida nyingi zinazoweza kukusaidia kupiga hatua zaidi katika maisha yako. Changamoto kubwa […]

by in MAISHA NA MALENGO, THAMANI

FAIDA ZA KUKIRI & KUKUBALI MAKOSA YAKO.

“Siku zote makosa yanaweza kusamehewa endapo tu mtu atakiri/kukubali kwamba amekosea.” Kila mtu hufanya makosa. Asilimia kubwa ya vijana wengi huogopa/huona aibu kukubali makosa waliyoyafanya kwa kudhani kwamba, huenda wataonekana dhaifu au kukosa msimamo. Wakati mwingine ni vigumu sana kukiri/kukubali makosa yako pale unapokosea na kitendo hiki kinaweza kuhitaji ujasiri na hekima ya kubwa sana. […]

by in MAISHA NA MALENGO, THAMANI

MAISHA YAKO YANAPATA UKAMILIFU KATIKA MAMBO YAPI? [CHUNGUZA UBORA WA MAISHA YAKO].

Habari za wakati huu Rafiki yangu. Pole kwa majukumu na harakati za siku katika kuhakikisha unaboresha maisha yako na kusogelea zaidi mafanikio. Napenda kuchukua fursa hii kukukaribisha tena katika ukurusa huu tuweze kujifunza pamoja na kuongeza zaidi THAMANI ya maisha yetu. Unaweza kuwa mtu wa aina yoyote katika maisha yako, unaweza kuchagua kuwa na kila […]