KUHUSU ANSELMO

ANSELMO JOHN NI NANI?

Anselmo John (au wengi hupenda kumuita Coach Ansey) ni Mwalimu, Mshauri na Mwandishi wa makala za Hamasa chini Tanzania hasa katika Masuala ya Kuhimili Hisia (Emotional Intelligence) na Maendeleo binafsi (Personal Development).

Kama Mwalimu na Mshauri, Anselmo amefanikiwa kufundisha na Kufikia zaidi ya Vijana 2000 kupitia Makala zake katika Mitandao ya Kijamii, Website, Semina na Madarasa maalumu yanayofanyika kupitia Makundi mbalimbali ya Whatsapp. Amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kugusa maisha ya vijana wengi, kuwasaidia katika kufanya mabadiliko chanya na kuongeza THAMANI zaidi katika maisha yao.

KUSAIDIA JAMII.

Kila Binadamu ana THAMANI kubwa sana kuwepo hapa duniani pasipo kuangalia Hadhi, Uchumi au Mazingira anayoishi. Kwa kuzingatia hili, Anselmo John ana shauku kubwa ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na wenye uhitaji. Yuko tayari Kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuleta Faraja, Furaha na Kuongeza Tabasamu  katika Maisha ya watoto wanaoishi katika mazingira hayo. Ana nia ya dhati katika kuhakikisha anakuwa chachu ya Mabadiliko chanya katika maisha ya watoto hasa wale wasiopewa THAMANI kama binadamu wengine. Je, unahitaji kuungana nae?

Kupitia Taasisi yake isiyo ya Kiserikali inayojulikana kwa jina la “HOPESTAR FOUNDATION” iliyoanzishwa na yeye mwenyewe, kila mwaka huandaa tukio Maalumu la kutembelea watoto katika maeneo mbalimbali ikiwemo;

  • Vituo vya kulelea Watoto Yatima.
  • Taasisi za Kielimu (Shuleni).
  • Magereza ya watoto.
  • Wodi za Watoto (Hospitali).

Unataka Kuongeza Furaha, Tabasamu na THAMANI zaidi katika Maisha yako? Hebu fikiria pale utakaposhiriki katika kumsaidia mtoto mmoja tu, aweze Kufurahi, Kutabasamu na Kuhisi kuthaminiwa. Alama utakayomuachia katika moyo wake, hatoisahau kamwe.

Anselmo anaamini kwamba, “Kila binadamu anastahili kupata Tabasamu na Furaha katika maisha yake kwa sababu yeye ni wa Thamani sana.”

Karibu tusaidiane katika kuifanya Dunia hii kuwa sehemu salama zaidi ya kuishi kuliko tulivyoikuta.

2300Wamepata Mabadiliko chanya.
200+Wanaotembelea ukurasa huu kila siku
7Nchi
team ya watu makini

TEAM YA THAMANI

Nyuma ya Majukumu mbalimbali ya Anselmo, wapo watu muhimu wanaoshiriikiana nae bega kwa bega katika kuhakikisha Vijana wa kitanzania wanafikiwa na Huduma hizi kwa urahisi na haraka zaidi.

Ally Hassan
Videographer

Founder & Marketing Manager at Beloved Brother Africa Brands.

Jacob Mushi
Web Developer

WordPress Site Developer & Founder of NetPoa.com

Mabadiliko ni Hatua. Katika kuhakikisha Anselmo anakuwa sehemu ya Utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakumba kundi kubwa la vijana hapa nchini na nje ya nchi, hii ni safari fupi tu aliyowahi kuipitia mpaka kufika hapa alipofika leo.

09April2017

Safari ya kutambua Kusudi lake Halisi.

Kila Binadamu amezaliwa akiwa na Kusudi flani la yeye kuletwa duniani. Kama binadamu wengine, Anselmo na yeye alianza kutafuta kujua ameletwa duniani ili kufanya nini?

14October2017

Kufahamu Kusudi lake.

Kwa msaada wa Mungu, Anselmo alifanikiwa kufahamu kusudi lake. “Ameletwa duniani ili kuwa Mwalimu (Kufundisha).”  Baada ya kujua kusudi hilo, alianza kutafuta eneo ambalo anaweza kufundisha na kutatua changamoto zinazowakumba vijana wengi katika eneo hilo.

Anselmo alipewa Maono ya kujikita zaidi katika Mambo yanayomgusa kijana juu ya “Maendeleo Binafsi (Personal Development) na Namna ya Kuhimili Hisia mbalimbali za Mwili katika maisha (Emotional Intelligence) hasa zikiwa ndio changamoto kubwa zinazoua na kudhoofisha ndoto za Kundi kubwa la vijana.

23October2017

Kufanyia kazi Kusudi lake.

Anselmo alifanya uamuzi sahihi kabisa wa kuanza kufanyia kazi kusudi lake pasipo kuogopa changamoto na vikwazo anavyoweza kukutana navyo njiani.

Alianza kwa kusoma Vitabu mbalimbali vinavyohusu maeneo hayo mawili aliyopewa maono ya kutafanyia kazi.

Kupitia Elimu yake ya Chuo kikuu aliweza kusoma kozi mbalimbali zilizomfundisha namna ya Kufanya mazungumzo mazuri na Vijana, Njia sahihi za kufundisha, Kushauri na kutatua changamoto mbalimbali za vijana Kisaikolojia na Kimwili.

Lakini vilevile, alipata nafasi ya kujifunza yeye mwenyewe kozi mbalimbali zinazotolewa na watu waliobobea katika fani zinazoshabihiana na maono yake kupitia Mtandao  wa internet (Self Learning).

Na huu ndio umekuwa msingi mkubwa wa ujuzi na umahili wake katika kazi zake mbalimbali.

01August2018

Kuanza Rasmi utekelezaji wa Kusudi lake.

Anselmo alianza rasmi safari yake ya Kufundisha na Kushauri vijana juu ya Maendeleo binafsi (Persinal Development) na Namna ya Kuhimili Hisia mbalimbali za mwili katika maisha (Emotiona Intelligence).

Alitengeneza Semina ya siku 30 iliyofanyika kupitia Mitandao yake ya kijamii (Instagram & Facebook). Semina hii aliita “SIKU 30 ZENYE THAMANI” na iligusa maeneo muhimu matatu,

  • Mabadiliko katika Maisha.
  • Thamani ya Muda katika maisha.
  • Thamani ya Mafanikio katika maisha.

Huo ndio ukawa mwanzo wa kutengeneza Brand yake ya “WEWE NI WA THAMANI”

26June2019

Maboresho Muhimu.

Ili kuwafikia vijana wengi, Anselmo alichukua uamuzi wa Kutengeneza Website ili aweze Kuandika Makala mbalimbali, kuweka Program na kozi mbalimbali zitakazosaidia katika kuongeza Maarifa na THAMANI zaidi katika maisha ya Vijana.

22October2019

Thamani Academy

Katika kuendana na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia, Anselmo (Coach Ansey kama wanavyomuita) alifanya uamuzi wa kuanzisha academy ya kidijitali (Digital Academy) ili kuwasaidia vijana Kujifunza, Kuelimika na kuongeza zaidi THAMANI katika maisha yao.

Academy hii inafahamika kama “THAMANI ACADEMY” inatoa Elimu, Ushauri na Mafunzo mbalimbali kwa njia mtandao. Mpaka sasa imeshaanza kufanya kazi kupitia mitandao ya kijamii (Instagram & Facebook), na vijana wengi sana wanaendelea kunuifaika kupitia Academy hii.

Thamani Acdemy inayosimamiwa na Kuendeshwa na Mwalimu Anselmo, imekuwa ni sehemu muhimu sana inayotegemewa na vijana wengi katika kupata Ushauri na Mafunzo mbalimbali yenye kuleta Matokeo chanya na Mabadiliko makubwa katika maisha yao.

Kuweka Malengo na Kuyatimiza kwa Wakati.
0
Kujenga NIDHAMU binafsi na Uwezo wa KuJIAMINI.
0
Kujenga MAHUSIANO Bora.
0
Kujenga FIKRA na MTAZAMO chanya.
0
Kuhimili HISIA mbalimbali za mwili.
0

UNATAFUTA MSHAURI KATIKA KUWEKA MALENGOKUJENGA MAHUSIANO BORAKUJENGA UWEZO WA KUJIAMINIKUJENGA FIKRA NA MTAZAMO CHANYAKUHIMILI HISIA MBALIMBALI ZA MWILI ILI KUONGEZA THAMANI ZAIDI KATIKA MAISHA YAKO?

KWANINI UNICHAGUE KUWA MSHAURI WAKO?

Mabadiliko chanya katika Maisha yako.
Kuongeza Zaidi THAMANI yako.
Matumizi sahihi ya MUDA wako.
Gharama Nafuu kabisa
Shuhuda

WATU WANASEMA NINI KUHUSU ANSELMO?